Matumizi Ya Visaiddizi Vya Ufundishaji Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Za Msingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya

Abstract

Utafiti huu ulishughulikia uchunguzi wa matumizi ya vifaa vya ufundishaji wa msamiati wa kiswahili katika shule za msingi za umma, Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki, Kenya. Malengo aliyozingatia mtafiti katika utafiti huu yalikuwa pamoja na kutambua changamoto zilizopo wakati wa kutumia vinyago, video na chati katika somo la msamiati katika somo la Kiswahili. Utafiti ulilenga idadi ya walimu kumi wa Kiswahili katika Shule za msingi katika Kaunti Ndogo ya Kisumu Mashariki. Baadhi ya hizi mtafiti aliteuwa kwa bahati nasibu walengwa walioteuliwa kama hivi walimu wakuu kumi, walimu wa Kiswahili kumi na wanafunzi kumi. Walengwa wote walikuwa mia nane ishirini ambao waliimbua asilimia kumi, basi idadi ilio hojiwa ikawa themanini na wawili. Hojaji zilikuwa tatu za walimu wakuu, walimu wa Kiswahili. Utafiti ulichanganuliwa kwa kutumia SPSS kuonyesha idadi katika alama za asilimia na uradidi. Baada ya kutafiti na kuchanganua data, mtafiti alipendekeza haja ya walimu wa Kiswahili kuwa na vikao katika majopo. Vivyo, wataweza kujadili na kutayarisha visaidizi wanavyohitajika kuboresha uelewekaji wa msamiati. Pamoja na hayo pia watauunda sera za kutengeneza visaidizi vya somo la Kiswahili zitakazowawezesha kupanga mikakati ya kukaguana wao kwa wao. Jambo hili litakuza umoja wa kufaana. Mtafiti pia aona kuwa kuna haja washika dau wote wa elimu kufufua taasisi za Kaunti ili kukuza hitaji la uundaji visaidizi ili walimu wapate kuendeleze ueledi wao wa kuunda visaidizi ili kuboresha uelewekaji wa dhana za Kiswahili. Kadhalika,washika dau wana changamoto kubwa ya kuleta mashuleni rasilimali ya kutosha kutengeneza visaidizi vinavyohitajika. Jambo lingine ni kuwa shule zingetenga sehemu mahususi ya kuhifadhi visaidizi ili vitumike bila uwoga wa kuharibika ama kupotea. Mwisho, walimu watie misingi thabiti ya ufunzaji msamiati kuanzia madarasa ya chini ili wanafunzi wasielewe dhana hizi kimakosa kisha wahitajike kurekebishwa baadaye. Jambo hili ndilo lililokita mizizi sehemu nyingi za Kaunti ya Kisumu Mashariki, Kenya.

Authors and Affiliations

Kamau Hellen Wambui

Keywords

Related Articles

V-SERVICE

Modern handheld devices such as smart phones and PDAs have become increasingly powerful in recent years. It mainly uses Android architecture. Android is the world's most popular mobile platform. It provides features like...

Design & Fabrication of ACV

Air Cushion Vehicle is a machine that can move on the land surface or water and it is supported by cushion that has high compressed air inside. The cushion is a closed canvas and better known as a skirt. An ACV moves on...

Homestead plant diversity in the south-central coastal saline region of Bangladesh: utilization and conservation

The present study has found a total of 189 plant species belonging to 152 genera and 74 families growing in homesteads in the south-central coastal region of Bangladesh. Despite variation of species diversity was found i...

Synthesis of Novel Pyrazole Derivatives by Vilsemeier Haack Reaction

A series of substituted carboxylic acid hydrazides on reaction with substituted acetophenone gave corresponding hydrazones which on Vilsmeier- Haack reaction resulted in corresponding formyl pyrazoles. The structures of...

Design and implementation of 4-bit Vedic Multiplier

Vedic mathematics is the name given to the ancient Indian system of mathematics that was rediscovered in the early twentieth century from ancient Indian sculptures (Vedas). This paper proposes the design of high speed Ve...

Download PDF file
  • EP ID EP244856
  • DOI -
  • Views 74
  • Downloads 0

How To Cite

Kamau Hellen Wambui (2016). Matumizi Ya Visaiddizi Vya Ufundishaji Msamiati Wa Kiswahili Katika Shule Za Msingi Za Umma, Kaunti Ya Kisumu Mashariki, Kenya. International journal of Emerging Trends in Science and Technology, 3(7), 4375-4385. https://europub.co.uk/articles/-A-244856